Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemtaka jaji kuu wa Tanzania kutumbua majibu kwa kuwafukuza kazi mahakimu wote walioshindwa kufikia masharti yaliyowekwa ya kutoa hukumu 260 kwa mwaka kwa kuwa wanachangia kuondoa sifa ya nzuri ya mahakama.
Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa mwaka mpya wa mahakama, Dkt Magufuli amesema bila ya kuchukua hatua hakuna kitakachofanyika kwa kuwa mambo yanayofanyika ndani ya serikali ni ya ajabu na yanaondoa sifa ya taifa la Tanzania.
Akizungumzia na viongozi wa serikali na taasisi za serikali wanavyofanya ufisadi wa fedha za walipa kodi Dkt Magufuli amesema.
Kuhusu udhahifu uliopo kwa upande wa ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka -DPPO- rais Dkt John Pombe Magufuli amesema haiwezekani mtuhumiwa anakamatwa na kidhibiti mikononi na kesi inachukua miaka kwa madai ya uchunguzi kutokamilika.
Kwa upande wake jaji mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Othumani Chande amesema mahakama inatarajia kuanza kusikiliza kesi za uchaguzi wa madiwani na wabunge kuanzia Februari 22 mwaka huu ambapo mashauri 221 ya kupinga matokeo ya uchaguzi yasikilizwa na jumla ya shilingi bilioni 3 zinahitajika, ambapo pia amesema mahakama iko katika mchakato wa kuanzisha mahakama maalum ya wahujumu uchumi na mafisadi.
0 comments:
Chapisha Maoni