Jumatano, Februari 24, 2016

NDEGE ILIYOPOTEA NEPAL, TARA AIR YAKUTWA IMEANGUKA NA KUUWA WOTE WALIOKUWAMO

Ndege iliyopotea nchini Nepal imekutwa imeanguka na abiria wote 18 na wahudumu watatu wamefariki.
Ndege hiyo aina ya Twin Otter ya Shirika la Ndege la Tara la Nepal ilikuwa inatoka Pokhara kuelekea Jomsom, na ilipoteza mawasiliano muda mchache baada ya kupaa.
Abiria wawili kati ya 18 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo ni wa kigeni, ambao wametambuliwa kuwa mmoja ni Mchina kutoka Hong Kong na mwingine ni raia wa Kuwait.

0 comments:

Chapisha Maoni