Jumatano, Februari 24, 2016

MWANAMKE ALIYEHUKUMIWA MIAKA 120 JELA COLORADO

Mwanamke mmoja,Dynel Lane,35,nchini Colorado amehukumiwa kifungo cha miaka 120 baada ya kupatikana na hatia ya jaribio la mauaji na mashambulizi ya kutumia kisu alipomdunga mwanamke mmoja mjamzito na kukata kijusu kutoka kwa mfuko wake wa uzazi.
Michelle Wilkins,27,ambaye alikuwa mwathirika alikuwa mjamzito wa miezi saba mwezi Machi mwaka jana,wakati aliona tangazo mtandaoni linalohusika na uuzaji wa vitu mbali mbali kwa kwenda nyumbani alikoishi Lane mjini Longmont,ambapo alishambuliwa na Lane na kuwachwa katika hali mahututi.
Lane alichukua kijusu hicho katika hospitali jirani baada ya kufanya mashambulizi hayo,akidai kuwa yeye alikuwa amepata ajali ya kuharibika kwa mimba lakini polisi walifanya uchunguzi na baadaye kumtia mbaroni.

0 comments:

Chapisha Maoni