Jumatano, Februari 24, 2016

KAMPALA NDIO SEHEMU POA ZAIDI KUISHI AFRIKA MASHARIKI

Utafiti wa shirika la Mercer unaonyesha kuwa mji wa Kampala nchini Uganda ndio bora zaidi wa kuishi katika kanda ya Afrika Mashariki.
Kampala iko kwenye nafasi ya 169 duniani Nairobi nambari 184, Kigali 191 na Dar es Salaam 198.
Cape Town iko nafasi ya 92 na Johannesburg 95.
Mercer imeitaja Vienna Austria kuwa mji bora zaidi wa kuishi duniani nayo Baghdad ikiwa ndio mji mbaya zaidi.
Utafiti huo uliangazia vigezo kama vile hali ya kijamii na uchumi, matishio ya ugaidi, afya, elimu, makaazi na mazingira.

0 comments:

Chapisha Maoni