Jumatano, Februari 24, 2016

KWANINI SULFUR DIOXIDE INATUMIKA KWENYE MVINYO?

Sulfur dioxide ni hatari kwa afya ya binadamu, lakini kwa nini inawekwa kwenye mvinyo? Tunahitaji kuangalia uzalishaji wa mvinyo kwanza.
Mvinyo unazalishwa kwa juisi ya zabibu. Sukari iliyomo ndani ya juisi hiyo ikichachuka, itabadilika kuwa kileo.
Lakini si kama tu chachu zinaishi ndani ya juisi hiyo, vijidudu vingine pia vipo. Hivyo tunahitaji kuviua vijidudu hivi ili kuzuia juisi ya zabibu isioze kabla ya mvinyo kuwa tayari.
Aidha, mchakato wa kuchachuka haumaliziki wenyewe mpaka sukari yote ibadilike na kuwa kileo. Tukitaka kuzalisha mvinyo wenye sukari, tunahitaji kusimamisha kazi ya kuchachuka mapema.
Hivyo kuua chachu au vijidudu ni hatua muhimu katika uzalishaji wa mvinyo. Lakini kuchemsha mvinyo si jambo zuri, kwa sababu hatua hii itaharibu ladha ya mvinyo.
Watu wamegundua kuwa Sulfur dioxide inaweza kukidhi haja ya kuviua vijidudu bila ya kuharibu ladha ya mvinyo. Kemikali nyingine zenye uhusiano na Sulfur dioxide pia zinaweza kufanya kazi hii, zikiwemo Sulfite, Pyrosulfite na Bisulfite. Kemikali zilizotiliwa kwenye mvinyo ni chache hivyo ni salama kwa afya.

0 comments:

Chapisha Maoni