Jumatano, Februari 24, 2016

KUNYWA KAHAWA KABLA YA KULALA HUAHIRISHA SAA YA KIBIOLOJIA YA BINAADAMU (Circadian Clock)

Utafiti mpya unaonesha kuwa kama mtu akinywa vikombe viwili vya kahawa ya aina ya espresso masaa matatu kabla ya kulala, saa yake ya kibiolojia itaahirishwa kwa saa moja hivi. Hii inamaanisha kuwa wakati wa usiku, watu hawafai kunywa kahawa, ama sivyo watakosa usingizi usiku na kushindwa kuamka wakati wa asubuhi.
Watafiti wa chuo kikuu cha Colorado nchini Marekani walishirikisha wanaume wawili na wanawake watatu katika majaribio. Katika muda wa siku 49, watu watano walitumia placebo au dawa zenye kafeini sawa na vikombe viwili vya kahawa ya espresso katika saa tatu kabla ya kulala.
Kila baada ya muda kadhaa, watafiti hao walipima kiwango cha melatonin, ambayo ni kitu muhimu kinachorekebisha saa ya kibiolojia ya binadamu. Matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa katika mazingira yenye giza, kwa kulinganishwa na watu wanaotumia placebo, saa ya kibiolojia ya wanaotumia dawa zenye kafeini iliahirishwa kwa dakika 40 hivi. Katika mazingira ya mwanga mkali, saa ya kibiolojia ya watu wanaotumia dawa zenye kafeini itaadhirishwa kwa dakika 105.
Hii ni mara ya kwanza kuthibitisha kafeini inaweza kuathiri saa ya kibiolojia ya binadamu.

0 comments:

Chapisha Maoni