Jumapili, Februari 21, 2016

NCHI MASKINI ZINAATHIRIWA ZAIDI NA TUMBAKU

Utafiti waonesha kuwa nchi maskini zinaathiriwa vibaya zaidi na tumbaku
Hivi karibuni utafiti unaonesha kuwa kwa kulinganishwa na nchi tajiri, sigara zinauzwa zaidi katika nchi maskini, na kuna matangazo mengi zaidi ya tumbaku.
Kuanzia mwaka 2009 hadi 2012, katika maskani 462 ya nchi 16 watafiti walihesabu matangazo na maduka ya sigara. Watu elfu 12 hivi walifanyiwa mahojiano kukumbuka kama waliangalia matangazo kupitia televisheni, redio au mtandao wa Internet au la katika miezi sita iliyopita.
Kwa mujibu wa takwimu, katika nchi zenye pato la wastani au chini ikiwemo China, Colomba na Iran, idadi ya maduka ya kuuzia sigara ni mara 3.5 ya nchi zenye pato la juu. Aidha, matangazo ya sigara ni mengi zaidi katika nchi zenye pato la chini ikiwemo India, Pakistan na Zimbabwe. Asilimia 10 ya watu waliohojiwa walisema waliona matangazo ya sigara kwenye aina zaidi ya tano ya vyombo vya mawasiliano katika miezi sita iliyopita.
Uvutaji wa sigara ni chanzo kikuu cha vifo vinavyowezwa kuepukika kote duniani. Shirika la Afya Duniani WHO limekadiria kuwa, kama hatua hazitachukuliwa, hadi kufikia mwaka 2020, uvutaji wa sigara utasababisha vifo vya watu milioni 8.4 duniani, na asilimia 70 ya vifo hivyo itatokea katika nchi zinazoendelea zenye wavutaji milioni mia 7 wa sigara.

0 comments:

Chapisha Maoni