Aliyekuwa gavana wa jimbo la Florida Jeb Bush amejiondoa kutoka kwa kinyanganyiro cha kiti cha Urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, baada ya kumaliza wa nne kwenye uchaguzi wa mchujo wa South Carolina ambapo mwanasiasa bwenyenye Donald Trump alishinda.
Bush ambaye alijibwaga ulingoni kuwania kiti hicho mwezi Juni mwaka uliopita sasa amepoteza katika majimbo ya Iowa, South Carolina na New Hampshire. "Watu wa Iowa, New Hampshire na South Carolina wameongea, nami nitaheshimu uamuzi wao," alisema Bush ambaye ni kakake rais wa zamani George W Bush na mwanawe Rais wa zamani George H W Bush. Bush alijipatia asilimia 8.1 ya jumla ya kura zilizopigwa katika mchujo huo wa South Carolina.
0 comments:
Chapisha Maoni