Jumatano, Februari 17, 2016

MPAKA SASA TANZANIA IMEPOKEA WAKIMBIZI 130,000 KUTOKA BURUNDI

Tanzania imepokea zaidi ya wakimbizi 130,000 kutoka kwa taifa la Burundi tangu mwezi wa April mwaka jana.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Isaac Nantanga, siku ya Jumanne, alisema kuwa wakimbizi hao walianza kufurika nchini humo mwaka jana, wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoanza nchini Burundi.
Bwana Nantanga, alieleza kuwa kati ya wakimbizi hao, 79,290 walikuwa katika kambi ya Nyarugusu na wengine 45,487 katika kambi ya Nduta, Kibondo.
Kambi ya Nyarugusu pia imewapa makazi wakimbizi 61,887 kutoka taifa la DRC Congo, 150 kutoka Somalia na 189 kutoka kwa mataifa mengine.

0 comments:

Chapisha Maoni