Jumamosi, Februari 27, 2016

MISIKITI NCHINI UHOLANZI YAPOKEA BARUA NZITO

Baraza la Misikiti nchini Uholanzi limetangaza kuwa, karibuni misikiti kumi ya nchi hiyo imepokea barua za vitisho.
Taarifa ya Baraza la Waislamu nchini Uholanzi imebainisha kwamba, viongozi wa misikiti hiyo wamesoma barua hizo na kukuta zikiwa na maneno ya vitisho na ya kuchukiza.
Baraza la Misikiti nchini Uholanzi limetoa wito wa kufuatiliwa kwa umakini mkubwa kadhia hiyo na limewataka Waislamu kutoa taarifa kwa polisi pindi watakaposhuhudia hatua au nyendo zozote zinazoonekana kufanyika dhidi ya misikiti na dhidi ya Waislamu.
Msemaji wa Baraza la Misikiti nchini Uholanizi ametangaza kuwa, baraza hilo lina matarajio kwamba, polisi itawatia mbaroni waliotuma barua hizo za vitisho dhidi ya misikiti nchini humo na mkono wa sheria kuchukua mkondo wake. Aidha amesema wanawataka viongozi wa nchi hiyo kuzingatia zaidi suala la usalama katika misikiti ya nchi hiyo.
Waislamu barani Ulaya wamekuwa wakiandamwa na vitisho na njama mbalimbali. Matukio ya chuki dhidi ya Uislamu yalishadidi zaidi barani Ulaya baada ya matukio ya Septemba 11 mwaka 2001.
Licha ya njama za kila upande dhidi ya Uislamu barani Ulaya, idadi ya watu wanaosilimu na kuingia katika dini hii tukufu imekuwa ikiongezeka kila siku katika nchi mbalimbali za bara hilo; jambo ambalo linaonesha kufeli njama za maadui dhidi ya Uislamu.

0 comments:

Chapisha Maoni