Jumamosi, Februari 27, 2016

KISIWA GHALI ZAIDI KUISHI DUNIANI NI THANDA CHA TANZANIA

Kisiwa cha Thanda kilichopo Tanzania Wilaya ya Mafia kusini mwa nchi, ndicho ghali zaidi duniani kwa binadamu kuishi, Gharama zake ni dola elfu kumi (10,000$) za kimarekani kwa siku sawa na Shilingi milioni ishirini za Kitanzania kwa siku.
Kisiwa hiki kinamilikiwa na kampuni ya utalii ya Zululand toka Afrika Kusini, ambapo kuna Hoteli yenye hadhi ya kidunia.
Haifahamiki kampuni hiyo inalipa kodi kiasi gani katika Serikali ya Tanzania, ama ilishauziwa eneo hilo la ardhi ya Tanzania. Taarifa isiyo rasmi inasema kuwa mmiliki wa kisiwa hicho amepewa hati ya umiliki/uwekezaji kwa miaka 66.

1 comments:

  1. Duuuuuuuu uo mkataba ni kwenye utawala wa naniiπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†

    JibuFuta