Jumapili, Februari 07, 2016

MAKAMISHNA WA TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR WAPINGA UCHAGUZI KURUDIWA

Makamishna wawili wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Ndugu NASSOR KHAMIS MOHAMED na AYOUB HAMAD wameibuika jijini Dar es salaam leo na kupinga marudio ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu kwa madai kuwa uchaguzi huo sio halali kulingana na matukio yaliyotokea tangu kufanyika kwa uchaguzi halali wa Oktoba 25 mwaka jana.
Wakizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam makamishna hao wamesema kuwa sababu kubwa ya kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo ni kutokana na kuvurugwa kwa katiba ya Zanzibar tangu tukio la kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana ambapo wamesema kuwa mwenyekiti wa Tume hiyo hakuwa na mamlaka ya kisheria kufuta uchaguzi huo bila kuwashirikisha makamishna wa tume hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni