Maganda na mbegu zina ladha mbaya, hivyo hakuna watu wanaopenda kuzila. Lakini utafiti mpya unaonesha kuwa kitu kinchoitwa Nomilin kilichoko ndani ya mbegu na maganda ya machungwa kinaweza kusaidia kupunguza uzito na kusaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu.
Kikundi cha watafiti cha chuo kikuu cha Tokyo, Japani kimeripoti kuwafanyia itafiti makundi mawili mawili ya panya, ambapo kundi la kwanza lililishwa chakula chenye mafuta mengi pamoja na nomilin, na kundi la pili lilipewa chakula chenye mafuta mengi tu. Baada ya siku 80, uzito wa panya wa kikundi cha pili uliongezeka kwa asilimia 10, na uzito wa panya wengine waliotumia nomilin haukubadilika.
Mbali na hayo kiwango cha sukari katika damu ya panya wa kikundi cha pili ilikuwa maradufu ya panya wa kawaida, lakini kiwango kile cha panya wa kikundi cha kwanza ni mara 1.5 ya panya ya kawaida.
Watafiti wanaendelea kutafiti jinsi ya kuinua ufanisi wa upatikanaji wa nomilin kutoka kwa maganda na mbegu ya machungwa.
Nimeipenda sana hii study.
JibuFuta