Wakulima wa mpunga katika skimu ya umwagiliaji Mawala kata ya Kahe wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamevamia na kuharibu miundombinu ya ugawaji maji kupeleka katika mashamba ya miwa ya mwekezaji wa kiwanda cha sukari TPC.
Wakulima hao wamesema wamelazimika kufanya uharibifu huo na kuelekeza maji katika mfereji wa mashamba ya wakulima kwa madai ya mwekezaji huyo kukausha maji yote mferejini na kuelekeza kwenye mashamba ya miwa hali ambayo imesababisha kusababisha mpunga uliopandwa kukauka kwa kukosa maji.
Wamesema wanasikitishwa na hatua ya mwekezaji huyo kukiuka makubaliano ya kugawana maji hayo kwa wiki siku tatu badala yake anatumia mashine ya kuvuta maji yote mferejini na kueleleza kwenye mashamba ya miwa hali ambayo imesababisha mashamba ya mpunga kukauka kwa kukosa maji.
Diwani wa kata ya Kahe mashariki Bw. Rodrick Mmanyi amelazimika kufika katika eneo la tukio na kuwataka wakulima kuacha kufanya vurugu na kuahidi kushirikiana na viongozi wa umoja wa wakulima hao ili kufanya mazungumzo na uongozi wa kiwanda cha sukari TPC kumaliza mgogoro huo ambao unahatarisha amani.
Hata hivyo juhudi za kumpata afisa utawala wa kiwanda cha sukari TPC Japhary Ally kuzungumzia mgogoro huo hazikufanikiwa baada ya kusema yuko kwenye kikao ambapo kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Ramadhani Mungi amesema amepata taarifa hizo na kwamba yuko safarini atatoa taarifa hizo kesho.
0 comments:
Chapisha Maoni