Takriban wanandoa 3000 kutoka kote duniani wameshiriki katika harusi ya halaiki katika makao makuu ya kanisa tata la kuwaunganisha watu Kusini mwa Korea.
Wengi wa wanandoa hao walikutana siku chache tu kabla ya kufungishwa ndoa na mamlaka ya kanisa hilo kabla ya sherehe hiyo ya jumamosi katika eneo la Gapyeong,kaskazini mashariki mwa Seoul.
Harusi hiyo ambayo hufanyika kila mara ilianza kufanyika miaka ya sitini.
Kanisa hilo lililoanzishwa na marehemu Sun Myung Moon, limeshtumiwa kwa kuwadanganya waumini wake,swala inalokana.
Sung Myung Moon alifariki mnamo mwezi Septemba mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 92.
Anaheshimwa na wafuasi wake wanaojiita Moonies.Wakosoaji wake wamemuelezea kuwa mtu muongo.
0 comments:
Chapisha Maoni