Ijumaa, Januari 08, 2016

WIVU WA MAPENZI WASABABISHA MUME KUMTIA KISU CHA KICHWA MKEWE

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Wajir nchini Kenya aitwae Fatma Ibrahim amechomwa kisu ubavuni mwa fuvu la kichwa na mumewe baada ya kutoelewana kati yao.
Taarifa iliyoambatana na picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, zinasema kuwa Madaktari wa Wajir walishindwa kumtibia mama huyo wa watoto wa 4 baada ya kugundua kuwa kisu kimenasa ndani ya fuvu la kichwa.
Mumewe aliyefahamika kwa majina ya Mohamed Deeq, alimshushia kipigo cha haja kabla ya kumtundika na kisu.
Fatma alisafirishwa na shirika la AMREF mpaka mjini Nairobi kwa matibabu na ufumbuzi zaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni