Tukio la kifo cha marehemu Steven Kanumba linaendelea kumwandama aliyekuwa mpenzi wake, Elizabeth “Lulu” Michael, kutokana na baadhi ya Watanzania kuendeleza tabia isiyokubalika, ya kumkejeli mwanaume yeyote anayesemekana kuwa na uhusiano naye kuwa kifo kinamuita.
Kitendo hicho kimejitokeza pia kwa muimbaji wa Nigeria, Tekno aliyedaiwa kuwa na uhusiano naye. Hata hivyo Lulu alikanusha na kudai kuwa huo ni uzushi kwasababu hakuna kinachoendelea kati yao.
Toka hit maker huyo wa ‘Duro’ arudi Nigeria amekuwa akipata comments nyingi kutokana na uzushi kuwa amenasa kwenye ulimbo wa Lulu, lakini kilichokuja kumchukiza zaidi ni comments za R.I.P zilizompelekea kuamua kufuta picha zake zote na kuandika ujumbe mrefu kuelezea Wanigeria na wengine wasioelewa sababu za comments za R.I.P kwenye ukurasa wake.
Haya ndio maelezo aliyopost Tekno ambayo baadae aliyafuta:
Kwa familia yangu, marafiki, bloggers na wote mliokuwa mkinipigia kuniuliza hizo comments za R.I.P zinamaanisha nini, kuna wanaosema kuwa nimetenda kosa la jinai nilipokuwa Tanzania! Lol.
Nilichokifanya mimi ni kupiga picha na msichana mrembo wa Tanzania sitamtaja jina lake. Kilichotokea ni kwamba wanaume wachache ambao waliwahi kuwa na uhusiano naye walifariki, kama wanavyosema!
Kwahiyo hawa watu wanaocomment R.I.P wanaamini kuwa nina uhusiano naye kwasabbu ya picha niliyopost Instagram ya mimi na yeye(Lulu), hivyo wanamaanisha na mimi nitakufa, wow! Inafurahisha.
Kwanza, nyie ni nani kuhukumu maisha yake,
Pili, nyie ni nani kucomment R.I.P kwenye ukurasa wangu…
Mungu tusamehe na utuangalie wote. Sasa mmefahamu.”
0 comments:
Chapisha Maoni