Ijumaa, Januari 08, 2016

GNAKO APIGWA $3000 (MILIONI 6) NDANI YA KIKAO CHA WASANII

Hivi karibuni kulikuwa na kikao cha wasanii wakijadili ishu yao ya malipo baada ya ngoma zao kuchezwa redioni,msanii G Nako aliibiwa dola elfu 3 katika mazingira ya kutatanisha. ‘’ G Nako kuna watu wamemwibia hela nilichomwambia angeangalia watu waliokuwa amekaa nao pale ni watu gani sasa yeye anasema aliokuwa amekaa nao ni ndugu zake,kama ameibiwa na ndugu zake tunashindwa kuingilia hiyo kesi ya ndugu,nimesikitishwa sana,’’Alisema Baba Levo.
Msemaji wa Kundi la Weusi Niki Wa Pili anaizungumzia ishu hiyo ilivyokuwa: ‘’ Ni dola elfu tatu kwahiyo huwezi kusema kama zimepigwa au ni kwamba G Nako alizipoteza katika mazingira ya kutatanisha tulikuwa kwenye kikao cha wasanii sasa sijui kuna mtu alichomoa au zilikuwa zimedondoka lakini kusema mtu ameiba itakuwa siyo sahihi kwa kuwa hatujui zimepoteaje,’’

HASSBABY MAPACHA

0 comments:

Chapisha Maoni