Ijumaa, Januari 08, 2016

KATI YA VIVUTIO VILIVYOPO MKOANI MBEYA NI PAMOJA NA MAPOROMOKO YA MAJI MWALALO


Ni maporomoko yanayopatikana katika safu za milima ya LIVINGSTONE karibu na kingo za ziwa Nyasa (MATEMA BEACH), kijiji cha Matema, wilaya ya Kyela mkoani Mbeya. Mto huu humwaga maji yake ziwa Nyasa.

Maporomoko haya yapo sehemu ambayo ni nzuri kwa (ku hike) ambapo huchukua takribani saa 1 (1hr) kutembea kwa mwendo wa kawaida (kwa miguu) kutoka katika kijiji cha Matema.

Ni nzuri kutembelea eneo hilo kwa muda wa ziada pale unapotembelea fukwe za ziwa Nyasa kwaajili ya mapumziko au sababu za kitalii kwa ajili ya zoezi la mwili, moja kati ya interesting moment ni pale katika kakilima ka mwisho kanakohitaji kupanda kwa kujivuta katika kamba.

Eneo lina sifa ya muonekano mzuri hasa wa rangi nyeupe ya maji yanayoporomoka katika miamba ya rangi ya mvuto ya kijivu.

Maporomoko haya yametengeneza bwawa zuri na la asili katikati ya miamba (mawe) ambacho ni kizuri kwa kuogelea, na kupigia picha

Pia maporomoko ya Mwalalo ni eneo zuri kwaajiri ya kupigia picha kutokana na muonekano mzuri uliopo hapo (Ungependa video ya msanii gani ingerekodiwa hapo?) Tuthamini na kuvitangaza vivutio vyetu.
Kwa nini usimuliwe? Karibu sana UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISES ujionee kwa macho yako na ujifunze mengi na kuburudika uwapo maeneo haya.wasiliana nasi kwa simu 0783545464/0766422703.

0 comments:

Chapisha Maoni