Rais wa Uruguay Tabare Vazques na yule wa Argentina, Mauricio Macri wamekubaliana kwa pamoja kuweka jitihada za kuandaa kombe la dunia mwaka wa 2030.
"Hii ndio nafasi mwafaka tumepata na tutajitolea ili tuweze kuwa wenyeji wa kombe la dunia mwaka wa 2030," Rais Macri alisema wakati wa mkutano wa pamoja na rais Vazquez katika makazi ya rais wa Anchorena.
Iwapo Uruguay itafanikiwa kuandaa kombe hilo mwaka wa 2030, itakuwa ni mara yake ya pili, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka wa 1930, ambapo nchi hiyo ilijipatia ushindi.
0 comments:
Chapisha Maoni