Jumamosi, Januari 09, 2016

WABUNGE WAPIGWA STOP KUTIBIWA NJE

Serikali imebana fursa ya safari za matibabu nje ya nchi kwa kuondoa urahisi uliokuwepo kwa maafisa wake na wabunge kupata kibali cha kwenda kutibiwa ughaibuni na hasa India.
Kwa sasa ni marufuku kwenda kutibiwa nje kwa maradhi ambayo yanaponyeka katika hospitali nchini.
Kwa sasa ili kwenda kutibiwa nje ya nchi, ni lazima mfanyakazi awe na matatizo ya kiafya ambayo matibabu yake hayapatikani nchini lakini pia safari yake italazimika kuidhinishwa na jopo la madaktari bingwa wa hospitali ya Muhimbili.
Awali watumishi wa Umma wakiwepo wabunge walikuwa wanapata idhini/ushauri wa kwenda kutibiwa nje ya nchi kutoka kwa daktari mmoja tu huku serikali ikibeba gharama kubwa za matibabu, nauli na posho kwa wale waliokuwa wakisafiri kwenda kupata matibabu huku wengine wakiambatana na waangalizi.

0 comments:

Chapisha Maoni