Wazazi watakaozembea kupeleka watoto wao shule kuanzia sasa, watahukumiwa kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya shilingi milioni 5.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu jana, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake.
Ummy Mwalimu alisema agizo hilo linatolewa katika kipindi ambacho Serikali inatekeleza Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008 inayosisitiza utoaji wa haki za msingi za mtoto ikiwamo ya kupata elimu.
0 comments:
Chapisha Maoni