Kanda ya video ya CCTV imetolewa ambapo daktari mmoja nchini Urusi alimpiga ngumi mgonjwa na kumuua.
Kisa hicho kilitokea katika mji wa Belgorod kilomita 670 kusini mwa mji mkuu wa Moscow mnamo mwezi Disemba tarehe 29.
Mgonjwa huyo alikuwa amempiga teke muuguzi mmoja kabla ya daktari huyo kumpiga ngumi ya kichwa kulingana na vyombo vya habari vya Urusi na kuzirai kabla ya kuaga dunia akiwa hospitalini.
Wachunguzi wanadhani kwamba hakumuua kwa makusudi lakini wameanzisha kesi ya uhalifu.
Habari hiyo ilisambaa baada ya kanda hiyo kutolewa.
0 comments:
Chapisha Maoni