Jumatatu, Januari 18, 2016

UJERUMANI KUWATIMUA WAHAMIAJI WA ALGERIA NA MOROCCO

Serikali ya Ujerumani imeweka mikakati mipya ya kuwafukuza wakimbizi wa Algeria na Morocco ambao wamekataliwa kuwa wakimbizi nchini humo.
Shirika la habari la Ufaransa limeripoti leo kuwa, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amefikia makubaliano na Horst Seehofer, mkuu wa eneo la Bavaria kwamba wakimbizi wa Algeria na Morocco ambao maombi yao ya kuwa wakimbizi yamekataliwa wapelekwe kwenye vituo maalumu.
Mkuu wa mrengo wa kisoshalisti katika bunge la Ujerumani naye amesema, hivi sasa ni jukumu la wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo kuongeza kasi ya kuchunguza maombi ya watu wanaoomba ukimbizi nchini humo na kurejeshwa walikotoka, wakimbizi wanaokataliwa.
Mwaka jana 2015, Ujerumani ilipokea karibu wakimbizi milioni moja na laki moja. Hata hivyo, mwezi Septemba mwaka jana, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ambaye kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni, umaarufu wake umepungua, aliahidi kufukuza idadi kubwa ya wakimbizi waliokimbilia nchini Ujerumani.

0 comments:

Chapisha Maoni