Mbeya ni kati ya mikoa ya Tanzania inayopitiwa na Bonde la ufa linalosadikika kutokea miaka 35 milioni iliyopita, bonde hili linatengeneza picha inayoonesha kuwa baada ya miaka kadhaa ijayo kupita, bara la Afrika litagawanyika kama ilivyo tokea miaka mingi iliyopita inayoaminika kuwa sayari ya dunia ilikua na bara moja lililojulikana kama PANGEA na kwa kutokana na mitikisiko iliyosababisha bara hilo kujigawa ikasababisha kutokea kwa mabara saba; hivyo basi tafiti za wana Jografia zinaonesha kuwa nchi za Afrika ya Mashariki zitajitenga/zitajigawa kutoka bara la Afrika na kutokea bara lingine.
Bonde hili la ufa limejigawa katika sehemu kuu ambazo ni: Upande wa Mashariki, Upande wa Magharibi na Upande wa Kusini
Upande wamashariki linaloanzia kuonekana katika nchi ya Syria (Magharibi mwa bara la Asia) kuelekea Kusini mpaka nyanda za juu Ethiopia, Somalia kuja Kenya kupitia ziwa Turkana; Mpakani na Tanzania kuna maziwa ya magadi kama Lake Natron. Ndani ya Tanzania baada ya kupita (mlima Kilimanjaro) bonde lapanuka hadi kutotambulika tena kwa macho. Kwenye (bonde la Usangu) linaonekana tena kama bonde lenye safu za milima kando.
La upande wa pili ni lile la Magharibi
huonekana vizuri kuanzia ziwa Albertna kuendelea katika maziwa ya ziwa Edward, ziwa Kivu, ziwa Tanganyika na ziwa Rukwa.
Upande wa Kusini Kusini ya Mbeya ufa inaendelea katika Ziwa Nyasa, halafu katika mabonde ya mto Shire na sehemu ya mwisho wa mto Zambezi hadi kuingia katika Bahari Hindi.
Mbeya ni sehemu pekee ambapo pande zote za bonde la Ufa zinakutana (Mashariki, Magharibi na Kusini).
Pia unaweza kuliona kwa uzuri bonde hili kupitia maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Mbeya, Lakini sehemu nzuri zaidi ni sehemu iitwayo RIFT VALLEY VIEWING POINT ambayo inapatikana katika eneo la misitu ya Kawetile barabara ya kuelekea Chunya, eneo hili ni zuri haswa kwa muonekano wake, hali ya hewa mwanana na linamuwezesha mtembeleaji kuona bonde la ufa kwa muonekano mzuri zaidi.
Pia eneo limetengenezwa vizuri kiasi kwamba linaweza kutumika katika kazi mbalimbali, kama kujifunza (study tour) sherehe tofauti tofauti kama Harusi na zingine, kupunga hewa, kupiga picha, kupumzika na zingine nyingi.
Ukitokea Mbeya mjini kuelekea eneo hilo utaweza kuona vitu mbalimbali kama; eneo maalum kwaajiri ya muonekano wa jiji (MBEYA CITY VIEWING POINT) katika sehemu hii utaweza kuiona sehemu kubwa ya jiji la mbeya, ukiendelea kupanda utaona Ofisi za hifadhi ya msitu wa Kawetile unaobeba historia kadhaa kama ukumbusho wa gereza la zamani, Barabara ya Uwanda wa Juu kuliko zote Tanzania yenye Altitude 2457M latitude 0835'S longitude 3325'E, Soko dogo la viungo (spice)na vyakula lililopo njiani, Kona kali sana iliyopewa jina la kona ya mkoa na vingine viingi saana na vizuri.
Nirahisi sana kuyafikia maeneo haya, wasiliana na UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISES, hawa watakuwa wenyeji wako katika kufurahia vivutio hivi hapa mkoani Mbeya,utawapata kwa simu 0783545464/0766422703.
Nirahisi sana kuyafikia maeneo haya, wasiliana na UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISES, hawa watakuwa wenyeji wako katika kufurahia vivutio hivi hapa mkoani Mbeya,utawapata kwa simu 0783545464/0766422703.
0 comments:
Chapisha Maoni