Jumatatu, Januari 18, 2016

TRUMP AALIKWA MSIKITINI AKAPEWE SOMO

Mkuu wa chama cha Leba cha nchini Uingereza, Jeremy Corbyn amemtaka Donald Trump anayewania kuteuliwa na chama cha Republican kugombea urais nchini Marekani atembelee msikiti mjini London, huenda akapata somo.
Amesema: Nimeamua kumwalika Donald Trump atakapotembelea Uingereza, afuatane na mimi hadi katika jimbo langu kwa sababu naona ana matatizo na Wamexico na Waislamu.
Corbyn amesema hayo baada ya kuzuka mjadala katika bunge la Uingereza wa kujadili iwapo Trump aruhusiwe kuingia nchini humo au la.
Mkuu huyo wa chama cha Leba cha Uingereza amesema, kwa mtazamo wake haoni haja ya kuzuiwa Donald Trump kuingia nchini humo, na iwapo atambelea Uingereza anapenda ampeleke msikiti akapate somo.
Amesema: Kama unavyojua, mke wangu mimi ni Mmexico na jimbo langu ni jimbo lenye watu wa makabila na tamaduni nyingi tofauti, sasa nitakachofanya ni kumchukua Trump hadi msikitini katika jimbo langu, ili aweze kuzungumza na watu huo.

0 comments:

Chapisha Maoni