Utangulizi
Nchi yetu ina kingo za mito na mabonde na maeneo
mengi hatarishi ambamo watu wanaishi kinyume cha sheria, huku wakiharibu
mazingira na kuhatarisha maisha yao. Kutokana na uhaba wa makazi, hali
ni mbaya zaidi katika mabonde ya Jiji la Dar es Salaam, hasa bonde la
Mto Msimbazi.
Serikali za awamu zote, zimekuwa zikifanya jitihada za kuwaondoa wakazi wa maeneo ya mabondeni wanaoishi katika maeneo hayo kinyume cha sheria lakini mafanikio yamekuwa si ya kuridhisha.
Serikali za awamu zote, zimekuwa zikifanya jitihada za kuwaondoa wakazi wa maeneo ya mabondeni wanaoishi katika maeneo hayo kinyume cha sheria lakini mafanikio yamekuwa si ya kuridhisha.

Kunusuru maisha ya wananchi wanaoishi katika mazingira hatarishi. Eneo
la Bonde la Mto Msimbazi lilitangazwa kuwa ni eneo hatarishi kuishi
binadamu tangu mwaka 1949 na baadaye 1979.
Kupanua uwezo wa mito
ya Dar es Salaam ili kupitisha maji ya mvua kwa kasi kubwa, hivyo
kupunguza uwezekano wa kutokea mafuriko na maafa wakati wa mvua nyingi;
Kuzuia milipuko ya magonjwa, hasa ya kipindupindu, hasa wakati wa mvua;
Kuzuia milipuko ya magonjwa, hasa ya kipindupindu, hasa wakati wa mvua;
Kuzuia eneo hilo kuendelea kutumika kama maficho ya wahalifu na uhalifu;
Kutoa nafasi kwa Serikali kuandaa na kuendeleza eneo hilo kwa mujibu wa sheria za nchi na mipango miji;
Utaratibu wa Zoezi
Utaratibu wa Zoezi
Kabla ya nyumba kubomolewa, taasisi hizi zinashirikiana kuhakiki iwapo
nyumba anayokaa mkazi ina nyaraka za umiliki na vibali vya ujenzi na
iwapo nyaraka hizo zina uhalali wowote. Nyumba ambazo zimethibitika
kuwepo katika maeneo yasiyostahili ndio zinawekwa alama X kuashiria
kwamba wakazi wanapaswa kuhama au kubomoa. Baada ya hapo, mkazi hupewa
muda wa kubomoa na kuhama mwenyewe.
Kutokana na utaratibu huu,
sehemu kubwa ya nyumba zinazobomolewa ni zile ambazo watu wamekwishaamua
kubomoa wenyewe. Baada ya hapo, alama huwekwa kuonyesha mpaka wa bonde.
Katika zoezi hili, imebainika kwamba sehemu kubwa ya wakazi wa maeneo
ya mabondeni ni wapangaji huku wamiliki wakikaa sehemu nyingine salama.
Serikali pia imeweka Dawati la Malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi.
Tathmini ya Zoezi
Jana, terehe 7
Januari 2016, Mawaziri watatu (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI; na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Makamu wa Rais; pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii), walifanya mkutano wa kutathmini zoezi la kuhamisha wakazi wa
mabondeni katika Jiji la Dar es Salaam.
Mkutano huo ulipokea
ripoti ya timu ya wataalam wa Wizara mbalimbali, inayoongozwa na Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, ambayo, pamoja na mambo
mengine ilibainisha kwamba sehemu kubwa ya kubaini makazi yaliyojengwa
kinyume cha Sheria katika Bonde la Mto Msimbazi imekamilika. Ripoti
ilieleza kwamba, hadi sasa, wananchi katika nyumba 774 wamehama na
nyumba hizo kubomolewa. Ilielezwa pia kwamba kabla ya mkazi kuombwa
kuhama, uhakiki kuhusu uhalali wa makazi anayoishi hufanywa. Kutokana na
uhakiki huo, jumla ya wakazi 20 walikuwa na hati halali za makazi na
wakazi 119 walikuwa na leseni za makazi za muda mfupi. Hawa watu
hawakuhamishwa. Mawaziri walipokea maelezo kuhusu changamoto mbalimbali
zilizojitokeza katika zoezi hilo. Baada ya tafakuri na mjadala,
Mawaziri hao walitoka na msimamo ufuatao, kama uamuzi wa Serikali: -
1. Zoezi la kuwaondoa wananchi waishio katika bonde la Mto
Msimbazi (eneo hatarishi) litaendelea kwa utaratibu ambao hautaleta
mateso na usumbufu kwa wananchi;
2. Katika awamu hii, zoezi litajikita katika Bonde la Mto Msimbazi tu.
3. Kwa wakati huu, watakaohitajika kuhama ni wale tu ambao makazi
yao yamo NDANI kabisa ya bonde, kwenye miteremko ya kuingia bondeni na
kwenye KINGO za mto;
4. Wale watakaokuwa na nyaraka halali
walizopewa na mamlaka za umma, zilizowamilikisha na kuwaruhusu kujenga
katika bonde hilo, hawatahamishwa bila kupewa sehemu nyingine za
kujenga. Na watumishi wa umma waliowamilikisha maeneo hayo watachukuliwa
hatua za kinidhamu na kisheria;
5. Serikali, ndani ya siku tatu zijazo, itaanza zoezi la kuzoa kifusi na kusafisha maeneo ambapo ubomoaji umefanyika.
6. Serikali itaheshimu amri za mahakama kuhusu mapingamizi
yaliyowekwa na baadhi ya wakazi wa mabondeni lakini pia itafuatilia kesi
hizi ziishe haraka ili taratibu zinazofuatia zifanyike;
7.
Serikali itawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wake wanaoendesha
zoezi hili kinyume na misingi ya sheria zinazotekelezwa, na kinyume na
misingi ya haki na uwazi, ikiwemo wanaoweka alama za X zaidi ya mita
zilizowekwa kisheria. Limeanzishwa dawati la malalamiko katika Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kupokea malalamiko au
maswali kuhusu zoezi hili.
8. Nyumba na majengo ya miaka
mingi, yaliyokuwepo miaka mingi kabla ya kutungwa kwa Sheria
zinazotekelezwa kwa zoezi hili, hayatabomolewa isipokuwa tu pale maisha
ya wakazi yapo hatarini. Wanaoishi katika makazi hayo watapewa miongozo
ya hatua za kuhifadhi mazingira na kujiokoa na maafa;
9.
Serikali haina dhamira ya kubomoa mahoteli makubwa ya siku nyingi yaliyo
karibu na fukwe katika maeneo ya Masaki. Wamiliki wa mahoteli haya
watapewa masharti na miongozo ya kuhifadhi mazingira kwa mujibu wa
Sheria.
10. Serikali inaweka uratibu wa karibu zaidi miongoni
mwa taasisi zake ili hatua za utekelezaji wa sheria za nchi zisiwe
chanzo cha taharuki katika jamii.
11. Serikali haina dhamira ya
kuwatesa wananchi wake kwa kuwalazimisha kuhama katika makazi yao bila
sababu za msingi. Lakini pia Serikali haiwezi kuruhusu wananchi
waendelee kukaa katika maeneo ambayo ikinyesha mvua kubwa maisha yao
yapo hatarini. Itakumbukwa kwamba katika mafuriko ya mwaka 2011,
wananchi 49 waishio mabondeni walipoteza maisha. Kwa mujibu wa taarifa
ya Kurugenzi ya Hali ya Hewa, mwaka huu zinatarajiwa kunyesha mvua kubwa
kuliko zilizowahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.
12.
Serikali inafuatilia kwa karibu kwa mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya
taarifa za wananchi wanaohitaji msaada maalum wa kibinadamu.
Suala la Mchungaji Getrude Rwakatare

Mwanasheria
huyo alificha makubaliano hayo kwa miezi mitano hadi Oktoba 2015,
yalipogundulika na mtumishi mwingine wa Baraza. Mkutano ulielezwa kwamba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kufuata taratibu zote,
alishaagiza kufukuzwa kazi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa
mwanasheria huyo. Mwanasheria huyo alifukuzwa kazi siku ya juzi tarehe 6
Januari 2016 na taarifa zake zimekwishafikishwa TAKUKURU. Vilevile,
Ofisi ya Makamu wa Rais, iliiagiza Baraza kufungua shauri mahakamani la
kuomba “makubaliano” kati yake na Mchungaji Rwakatare yawekwe pembeni
kwasababu yalipatikana na njia ya udanganyifu. Shauri hilo lilifunguliwa
tarehe 29 Disemba 2015.
Kuhusu Karakana ya Mradi wa Mabasi Yaendayo kwa Kasi (DART)
0 comments:
Chapisha Maoni