Alhamisi, Januari 07, 2016

SERIKALI YASITISHA SAFARI ZA MV SERENGETI

Serikali imelazimika kusitisha safari za meli ya Mv Serengeti kwa muda wa siku tatu ili kupisha hatua ya matengenezo kutokana na hitilafu iliyojitokeza juzi katika mfumo wa shafti na majembe ya upande wa kulia wa meli hiyo.
Meli ya MV Serengeti inadaiwa kupata hitilafu juzi Januari 5 mwaka huu baada ya kunaswa na nyavu wakati ikiwa safarini kutoka Mwanza kwenda Bukoba ikiwa na abiria 269 na tani 64 za mizigo hali iliyosababisha madahara yaliyopelekea injini ya meli hiyo kuwa nzito.

0 comments:

Chapisha Maoni