HABARI njema ikufikie: Staa wa muziki nchini Marekni, Rick Ross “Rozay” ameendelea kujipanua kikazi mwaka huu mpya wa 2016. Rozay ameamua kuachana na kampuni ya muziki aliyokuwa akifanya nayo kazi tangu mwaka 2006 ya Def Jam na kupata dili nono kwenye kampuni ya Epic Records.
Picha za Rozay alizoweka kwenye akaunti yake ya twitter wikiendi iliyopita zilimuonesha yeye na Mkurugenzi wa Epic Records, L.A. Reid pamoja na msaidizi wake Sylvia Rhon huku Rozay akiandika: “Welcome @rickyrozay to the #EPIC family!”
Rozay alisaini mkataba na kampuni ya Def Jam mwaka 2006 na kufanya albamu nane kwenye lebo hiyo ya Epic kuanzia kipindi hicho mpaka anapoondoka kwenye kampuni hiyo. Albamu yake ya mwisho kufanya na Def Jam ni ile aliyoiachia Decembere mwaka jana ya Black Market, ambayo inatamba na kushika namba 6.
Rozay amejiunga na wasanii kibao walioko kwenye lebo ya Epic wakiwemo; Future, Diddy, Mariah Carey, Ciara, Travis Scott na Fifth Harmony.
Ross pia anadili jingine na Warner Music kwa ajili ya Maybach Music Group yenye wasanii wakali kama Meek Mill, Wale, Stalley, Rockie Fresh na Omarion. MMG pia anahusishwa kuhamia Epic Muda wowote.
0 comments:
Chapisha Maoni