RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amemtumia salam za pongezi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye kufuatia mchezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa
miguu (Taifa Stars) Mbwana Ally Samatta kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa
Afrika kwa wachezaji wanaocheza Barani Afrika; iliyotolewa katika mji
wa Abuja nchini Nigeria jana usiku.
Mhe. Rais Magufuli amemtaka
Waziri Nape Nnauye amfikishie salam zake za pongezi kwa mchezaji huyo
ambaye pia ni mchezaji wa kulipwa wa TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo DRC) .
Amesema tuzo hiyo imemjengea heshima
na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa nchini na
Tanzania kwa ujumla katika medani ya Soka Kimataifa.
Aidha, Rais
Magufuli amewasihi wachezaji wa soka wote na wadau wa mchezo huo
kuongeza juhudi za kuundeleza mchezo huo ili upige hatua zaidi za
kimaendeleo.
0 comments:
Chapisha Maoni