Ili kupunguza ongezeko
la vitendo vya uhalifu unaohusisha silaha wananchi mkoani Iringa wameshauriwa
kusalimisha kwa jeshi la polisi silaha zao wanazozimiliki kinyume cha sheria.
Akizungumza na
waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani
Mungi amesema kuwa ni vyema wananchi wanaomiliki silaha bila kibali wakazisalimisha
katika vituo vya polisi au kwa viongozi wa serikali za mitaa.
Ameongeza kuwa kwa sasa
jeshi la polisi mkoa wa Iringa limeanzisha msako mkari wa kuhakikisha kuwa linawakamata
watu wote wanaomiliki silaha pasipo kuwa na kibari hali itakayo pelekea
wananchi wa mkoa wa Iringa kuishi kwa usalama kwa maisha yao pamoja na mali zao.
Kamanda Mungi amesema kuna
baadhi ya wananchi ambao wanamiliki silaha ambazo wamezirithi kutoka kwa ndugu
zao ambapo amewataka kufuata taratibu za husika za kisheria ili kupata kibari
cha umiliki wa wa silaha hizo.
Aidha amesema licha ya
kuwepo kwa wananchi wanaomilili silaha kinyume cha sheria pasipo kuwa na kibari
maalumu pia ameongeza kuwa kuna tatizo la baadhi ya wanaomiliki kihalari silaha
hizo wanazitumia kwa matumizi ya kihalifu.
0 comments:
Chapisha Maoni