Akizungumzia tukio hilo Balozi wa mtaa huo Ndugu Ezekiel Mwakalundwa
amesema kuwa amepata taarifa za kupatikana kwa mwili wa mtoto huyo
majira ya saa 1 na nusu asubuhi kutoka kwa majirani waliokuwa karibu na
eneo.
Amesema baada ya kupata taarifa hizo aliongozana na majirani pamoja
na baadhi ya ndugu wa marehemu huyo hadi eneo la tukio ambako kitendo
hicho cha kikatili I,mefanyika na kukuta mwili wa mtoto huyo ukiwa
umelazwa ndani ya sinki la kuogea ndani ya moja ya chumba kwenye pagale
hilo huku ukiwa hauna nguo.
Amesema mara baada ya kuupekua mwili huo waligundua kuwa mtoto huyo
aliofanyiwa vitendo vya kikatili kuwa alibakwa ambapo sehemu zake za
siri zilikuwa zimeharibika bibaya na tayari mwili wake ulianza
kuharibika na kuanza kutoa harufu.
Amesema mara baada ya kushuhudia tukio hilo alitoa taarifa katika
kituo cha polisi kati ambapo polisi walifika na kuchukua mwili wa
marehemu huyo ma kupeleka katika hospital ya rufaa kwa ajili ya
kuafanyiwa uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.
Amesema kutokana na mazingira yaliyonekana katika eneo hilo huenda
binti huyo alibakwa hadi kufa kwani sehemu zake za siri zilikuwa
zimeharibika vibaya.
Kwa upande wao majirani wanao ishi karibu na eneo hilo wamedai kuwa
tukio la kuwawa kwa mtoto huyo si tukio la kwanza kwani matukio ya aina
hiyo yamewahi tokea zaidi ya mara tatu yakihusisha kubwakwa kwa watoto
wadogo.
Mmoja wa majirani hao aliyejitambulisha kwa jina la Kristina
Mwakalundwa amesema tukio hilo ni la tatu kutokea ambapo kuna mapagara
pamoja na miti ya mianzi ambayo ndio imekuwa chanzo cha kufanyikakwa
matuki hayo ya ubakaji.
Amesema chanzo kingine cha tukio hilo kunatokana na baadhi ya
wananchi kupanda mahindi pembezoni mwa makazi ya watu ahali ambayo
imekuwa ikichangia kwa kiwango kikubwa kutoa mianya ya wahalifu kufanya
vitendo vya kinyama vinavyo fanana na tukio hilo .
Kufuatia tukio hilo ameitaka serikali pamoja na wakazi wa eneo hilo
kuungana kwa pamoja kuhakikisha wanapinga hatua ya baadhi ya watu
kuendeleza shughuli za kilimo pembezoni mwa makazi ya watu.
Akizungumzia kwa masikitiko makubwa mama mlezi wa mto to huyo Ndugu
Sala Mwandobo amesema binti yake alitoweka nyumbani toka jana January 7
mwaka huu nakwamba aliaga nyumbani kuwa anakwenda kufua nguo za shule
eneo la chemchem ya maji mita kadhaa toka nyumabni anako ishi mtoto
huyo.
Akielezea zaidi mama huyo amesema kuwa yeye alikuwa safari na kwamba
alirudi jana hiyohiyo ambapo mara baada ya kurudi nyumbani alimkuta
binti huyo akiwa na sare za shule majira ya saa 9 mchana baada ya
kulejea kutoka shule ambapo mtoto huyo alikunywa chai kisha kumuomba
mama yake kuwa anataka kwenda kufua nguo kwani zimeloa ambapo alimruhusu
na kumtaka awahi kurudi nyumbani .
Amesema baada ya mtoto huyo kuondoka alichukua muda mrefu hali ambayo
ilizua hofu nyumbani kwako ambapo mama huyo aliagiza wenzankle kumfuata
ikiwa majira ya saa 11 jioni ambapo hata hivyo hawakuweza kufanikiwa
kumpata hivyo waliamua kutoa taarifa kituo cha polisi ilomba majira ya
saa 1 jioni .
Amesema baada ya kutoa taarifa hizo kituo cha polisi waliendelea
kutoa taarifa pia kwa majirani huku wakiendelea kumtafuta hadi ilipo
fika midaa ya saa6 usiku ambapo walikata taamaa na kurudi nyumbani.
Amesema ilipo fika asubuhi ya leo majira ya saa1 asubuhi walipata
taarifa za kukutwa kwa mtoto akiwa amekufa ndani ya pagale jirani na
nyumbani kwao.
Amesema baada ya kwenda kushuhudia mwili huo waligundua kuwa ni mtoto
wake ambapo alikutwa akiwa na ndoo pamoja na nguo alizokwenda kufua
huku akidai kuwa yawezekana watu hao waliofanya kitendo hicho
walimkamatia maeneo hayo kabla ya kufika eneo la kufulia nguo.
Amesema inasikitisha sana na inamuuma sana kwani binti huyo
alimchukua kwa mdogo wake kijijini akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu
akiwa katika hali mbaya ya kiafya ambapo mapaka sasa umauti unamkuta
mtoto huyo
Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa mbeya ahmed Msangi
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwili wa motto huyo
umehifadhiwa katika hospital ya rufaa mbeya kwa ajili ya uchunguzi
zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni