Ijumaa, Januari 01, 2016

HERI YA MWAKA MPYA 2016

Leo ni tarehe Mosi Januari inayosadifiana na kuanza mwaka mpya wa 2016 Miladia. Mpangilio wa miezi ya mwaka wa Kirumi unaoanza Januari hadi Disemba ulianza kutumiwa katika kipindi cha Mfalme Numa Pompilius yapata miaka 700 kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo. Kwa msingi huo tarehe 31 Disemba huwa siku ya mwisho ya mwaka wa Miladia na usiku wa kuamkia tarehe Mosi Januari huanza sherehe za kupokea mwaka mpya katika jamii za Wakristo na nchi nyingi za Afrika, America, Ulaya, Australia na hata Asia.

0 comments:

Chapisha Maoni