Mchezo namba 27 wa Ligi Kuu ya Vodacom uliowakutanisha watani wa jadi
Young Africana kutoka eneo la Jangwani na Simba SC kutoka eneo la
msimbazi jijini Dar es salaam umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana
(0-0), mtanange uliofanyika jioni ya leo kwenye dimba la Uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Young Africans ilingia uwanjani
chini ya kocha wake Marcio Maximo kusaka pointi tatu hali kadhalika
Phiri wa Simba akisaka alama tatu pia hali iliyopelekea mchezo huo kuwa
mgumu kutikisika kwa nyavu za pande zote mbili.
Kocha
mbrazil alimtumia mshambuliaji Jaja akisaidiwa na Coutinho, Ngasa,
Niyonzima na viungo Mbuyu Twite na Hassan Dilunga huku Phiri akimtumia
Maguri kama mshambuliaji kiongozi akisaidiwa na Kiemba, Ndemla, Chanongo
na Okwi.
Young Africans
ilifanya mashambuizi kadhaa langoni mwa Simba kupitia kwa washambuliaji
wake hali kadhalika wapinzani nao walifanya hivyo pia lakini
mashambulizi ya timu zote mbili yalikuta yakiishia mikononi kwa walinda
mlango wa timu zote.
Mpaka dakika 45 z akipindi cha kwa kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Simba SC.
Kipindi
cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko kwa lengo la kusaka
bao la mapema katika mchezo wa huo, lakini kutokua makini kwa
washambuliaji wa timu zote kulifanya milango kuendelea kuwa migumu
kufunguka.
Andrey Coutinho alikosa nafasi mbili za kuipatia Young
Africans bao baada ya kupokea krosi nzuri ambazo alishindwa kuzitumia
vyema kuukwamisha mpira wavuni na kukuta michomo yake ikiokolewa na
mlianda mlango wa Simba SC Manyika Peter.
Simba ilifanya
mashmabulizi langoni wa Young Africans kupitia kwa washambuliaji wake
Okwi, Maguri na Chanongo lakini jitihada zao hazikuzaa matunda na kukuta
mipira yao ikiishia mikononi wa mlinda wa Deo Munish "Dida" na mingine
kupaa juu ya lango au kuokolewa na walinzi.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Simba SC.
Young Africans:
1. Dida, 2. Juma Abdul/Telela, 3. Oscar, 4. Cannavaro, 5. Yondani, 6.
Twite, 7.Dilunga, 8.Niyonzima/Msuva, 9.Jaja/Kizza, 10.Ngasa, 11.
Coutinho
Simba SC: 1. Manyika, 2. Gallas, 3.
Mohamed, 4. Isihaka, 5. Owino, 6.Mkude/Seseme, 7.Chanongo,
8/Ndemla/Kisiga, 9.Maguri, 10.Kiemba/Messi, 11.Okwi
0 comments:
Chapisha Maoni