Miaka 62 iliyopita, Dakta Hussein Fatimi, Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya Dakta Muswadiq, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Iran wakati huo alitangaza kukatwa uhusiano wa kisiasa kati ya Iran na Uingereza. Uamuzi huo ulikabidhiwa kwa balozi mdogo wa Uingereza mjini Tehran, baada ya kuidhinishwa na baraza la mawaziri. Dakta Fatimi alisema Tehran imeamua kukata uhusiano na Uingereza kutokana na upuuzaji wa serikali ya London kwa matakwa ya wananchi wa Iran ya kujipatia haki zao, hususan katika uwanja wa kutaifisha sekta ya mafuta. Dakta Fatimi aliwataka viongozi wa London wabadili siasa zao kuhusiana na Iran.
Na miaka 58 iliyopita katika siku kama hii ya leo, mawaziri wakuu wa Ufaransa, Uingereza na utawala wa Kizayuni wa Israel walichunguza mpango wa kuivamia Misri katika kikao cha siri kilichofanyika Ufaransa. Ufaransa na Uingereza ziliazimia kuukalia kwa mabavu mfereji wa Suez baada ya kupoteza maslahi yao haramu katika eneo hilo, kufuatia tangazo lililotolewa na Rais Gamal Abdulnasir wa Misri mwaka 1957 la kutaifisha mfereji huo.

0 comments:
Chapisha Maoni