Klabu za Bayern Munich, Chelsea pamoja na Shakhtar Donetsk zimeweka
rekodi ya kufunga mabao mengi katika nusu ya kwanza ya michezo ya hatua
ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Klabu hizo tatu zimefanya hivyo usiku wa kuamkia hii leo katika
michezo ya mzunguuko wa tatu ambapo FC Bayern Munich walikuwa ugenini
mjini Roma nchini Italia, wakipambana na AS Roma ilihali Shakhtar
Donetsk walikuwa nyumbani mjini Donetsk nchini Ukraine wakicheza dhidi
ya BATE Borisove huku Chelsea wakicheza nyumbani Stamford Bridge dhidi
ya NK Maribor kutoka nchini Slovenia.
FC Bayern Munich pamoja na Shakhtar Donetsk ziilifanikiwa kuacha
vilio kwa wapinzani wao kufuatia ushindi wa mabao saba waliouvuna na kwa
upande wa Chelsea waliibuka na ushindi wa mabao sita kwa sifuri na
hivyo kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kuichungulia nafasi
ya kutinga katika hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya abingwa barani
Ulaya msimu huu.
Katika mchezo wa FC Bayern Munich dhidi ya AS Roma mabao ya mabingwa
hao kutoka nchini Ujerumani yalifungwa na Mario Goetze, Robert
Lewandowski, Thomas Mueller, Xherdan Shaqiri, Franck Ribery pamoja na
Arjen Robben aliyefunga mabao mawili.
Bao la AS Roma katika mchezo huo lilipachikwa wavuni na mshambuliaji
kutoka nyumbani Afrika katika nchi ya Ivory Coast Gervais Yao Kouassi
Gervinho.
Kwa upande wa Shakhtar Donetsk mabao yao yalifungwa na Alex Teixeira,
Douglas Costa pamoja na Luiz Adriano aliyefunga mabao matano.
Chelsea mabao yao yalipachikwa wavuni na Loic Remy, Didier Drogba,
John Terry pamoja na Eden Hazard aliefumnga mabao mawili huku Mitja
Viler akijifunga mwenyewe.
Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo ni kwamba
Schalke 04 4 - 3 Sporting CP
FC Porto 2 - 1 Athletic Bilbao
APOEL Nicosia 0 - 1 Paris Saint Germain
Barcelona 3 - 1 Ajax
CSKA Moscow 2 - 2 Manchester City
0 comments:
Chapisha Maoni