Rais wa Marekani, Barack Obama,
ametoa kauli yake kuhusu mwanamume aliyeshikwa na wivu baada ya yeye
kumbusu mpenzi wake kwenye mashavu.
rais tafadhali usimguse mpenzi wangu
alisema mwanamume, aliyetambuliwa na CNN kama Mike Jones.
Yote
hayo yalitokea wakati Obama alipokuwa anapiga kura ya mapema katika
jimbo la Illinois karibu na mwanamke aliyetajwa tu kama Aia Cooper.
Kusema kweli sikuwa nimepanga kufanya hivyo
alisema Rais Obama , huku
akiendelea kupiga kura yake huku Copper akiangua kicheko.
Baadaye Copper aliyeonekana kushikwa na aibu aliomba radhi kwa niaba ya mpenzi wake.
Obama
alionekana naye kashikwa na aibu na kusema kwa tabasamu kuwa
hiki ni kisa tu cha mwanamume ndugu yangu kutaka tu kuniabisha bila sababu
Baada
ya maongezi ya muda mfupi kati ya Obama na Cooper, wawili hao
walimaliza kupiga kura, na kamera ikaonyesha Obama akimbusu Cooper
mashavuni na kumpa mpenzi wa Coopper sababu nyingine ya kuongea.
0 comments:
Chapisha Maoni