Jumatatu, Oktoba 27, 2014

RAIA AKAMATWA NA SHORTGUN NA RISASI 7 MBEYA

Mtu mmoja aitwaye Emanuel Mwakeja (27) mkazi wa Pambogo – Airport alikutwa akiwa na silaha bunduki moja aina ya Shortgun ikiwa na risasi saba [07] nyumbani kwake baada ya kupekuliwa.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa jana saa 12:40 jioni huko Pambogo, kata ya Iyela, tarafa ya Iyunga, jiji na mkoa wa Mbeya.
Inadaiwa kuwa, tarehe 26.10.2014 majira ya saa 11:45 huko maeneo ya uwanja wa Sokoine, kata na tarafa ya Sisimba, jiji na mkoa wa Mbeya mtu mmoja aitwaye Alfonce Mwakasege (38) mkazi wa Makunguru aligundua kuibwa kwa pikipiki yake yenye namba za usajili T.683 BDM aina ya Kinglion na kufanikiwa kuwakamata watu wawili ambao ni 1. Joseph Kigulu (24) mkazi wa Airport na 2. Juma Nelson (31) mkazi wa Iyela.
Watuhumiwa hao baada ya kukamatwa na kuhojiwa walidai kuwa pikipiki hiyo ipo nyumbani kwa Emanuel Mwakeja na walipokwenda waliikuta nje na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.
Mtuhumiwa huyo alipekuliwa nyumbani kwake na ndipo alikutwa na silaha bunduki moja aina ya short gun na risasi saba ikiwa imewekwa chini ya godoro chumbani kwake.

0 comments:

Chapisha Maoni