Jumanne, Oktoba 21, 2014

PISTORIOUS JELA MIAKA 5

Mahakama ya Afrika Kusini imemhukumu kifungo cha miaka 5 jela mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Mwezi September, mahakama hiyo ilimkuta Pistorius na hatia ya kumuua Reeva Steenkamp bila kukusudia katika siku ya wapendanao mwaka jana (February 14,2013).
Pistorius alikiri kumpiga risasi Reeva nyumbani kwake na kujitetea kuwa alidhani ni mtu aliyevamia nyumbani kwao usiku ule.
Akitoa masharti ya hukumu hiyo, jaji ameeleza kuwa Pistorius anapaswa kutumikia angalau 1/6 (Miezi 10) ya adhabu yake kabla hajafikiriwa kwa lolote.

0 comments:

Chapisha Maoni