Mkurugenzi wa LINO International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga hii leo amezungumza na waandishi wa habari juu ya sakata la umri halali wa Mrembo alietwaa taji hilo Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu.
Lundenga amelitolea ufafanuzi suala la umri wa mrembo huyo kulingana na vilelezo alivyopewa na Sitto Abbas Mtemvu wakati akijiunga na mashindano hayo
Katika mashindano yetu, Washiriki wote hujaza fomu maalum zilizoandaliwa na Kamati ya Miss Tanzania. Katika fomu alizojaza mrembo wa Miss Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu amejaza tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni Mei 31,1991 na hivyo kuwa ni sahihi kushiriki mashindano yetu
Alisema Lundenga mbele ya wanahabari hao.
Lundenga aliendelea kusema kuwa Mashindano ya Miss Tanzania hayaruhusu mshiriki yeyote mwenye mtoto kushiri,hivyo katika suala la Sitti Mtemvu kuwa ana mtoto,hilo kalina ukweli wowote bali ni uvumi tu wa kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mrembo huyo kuonekana akiwa katika picha na mtoto alieomba kupiga nae.
Hata hivyo, maswali ya waandishi wa habari kwa Miss Tanzania yalizua utata mwingine baada ya kuonekana cheti kilichooneshwa kwa waandishi hao kimetengenezwa September mwaka huu.
Waandishi walihoji kuhusu cheti chake cha kuzaliwa cha awali ambacho alikitumia kupata passport na leseni ya udereva, mrembo huyo alisema cheti hicho kilipotea na alitoa taarifa polisi. Waandishi hao walipotaka kujua kituo cha polisi alichoripoti upotevu wa cheti hicho, alisema hataki kuzungumzia suala hilo.

0 comments:
Chapisha Maoni