Jumanne, Oktoba 21, 2014

MADEREVA BODABODA IRINGA WALILIA MIKOPO

Waendesha boda boda‭ ‬wa‭ ‬Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa wameiomba Serikari kuwawezesha mikopo ya kupata boda boda kwa riba nafuu ili kuondokana na tatizo la ajira na kujiajili wenyewe.
Mwenyekiti wa chama cha waendesha boda boda Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa Bw.Joseph Mwambope amesema hayo kwa niaba ya waendesha boda boda walipokutana na Naibu Waziri wa Maliasili Mh January Makamba katika ofisi zao.
Bw.‭ ‬Mwambope ameongeza kuwa idadi kubwa ya madereva wa bodaboda wanaendesha boda boda zisizo zao na kupelekea kushindwa kujikimu katika maisha yao kwa sababu ya kupeleka pesa nyingi kwa waajili wao.
Kwa upande wa Naibu Waziri wa Mawasiliano Mh. January Makamba amekubali kuwasaidia‭ ‬kwa‭ ‬kuwakutanisha na‭ ‬kuwaunganisha na watu ambao wanatoa mikopo ya boda boda kwa riba nafuu na kuwaomba viongozi kushughulikia jambo hili kwa kusaidiana nao.
Hata hivyo Mh. Makamba amewataka waendesha boda boda wa Manispaa ya Iringa kuondokana na vitendo vya kiharifu ambavyo vinatokokana na waharifu hao kuutumia usafiri huo ama wao wenyewe kujihusisha kwenye vitendo hinyo.

0 comments:

Chapisha Maoni