Diamond Platnumz ambae kwenye birthday yake hivi karibuni management
yake ilimzawadia gari aina ya BMW X6 ambapo inaaminika amechukua namba
hizi kwa ajili ya mkoko wake aliozawadiwa na atakua msanii wa kwanza
kuweka jina lake badala ya namba kwenye gari.
Utaratibu wa kuweka majina badala ya namba umeanza kutumika kihalali
nchini Tanzania ambapo watu mbalimbali wasio maarufu walishaanza
kujiwekea miezi kadhaa iliyopita ambapo ada yake ni milioni tano kwa
miaka mitatu.
0 comments:
Chapisha Maoni