Msanii wa muziki wa hip hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benzi’ anaendelea
kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukamatwa na dawa za
kulevya na kesho anatarajiwa kufikishwa mahakamani. Chidi Benzi alikamatwa na dawa za kulevya juzi jioni katika Uwanja wa
Kimataifa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam wakatia wa ukaguzi kabla
ya kupanda ndege ya Fastjet akija jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya
Tanzania, SACP Alfred Nzowa, msanii huyo ameendelea kushikiriwa na jeshi
la polisi mpaka kesho atakapofikishwa mahakamani.
Alisema Chidi Benz alikamatwa na dawa aina ya Heroine kete 14 na
misokoto miwili ya bangi, vyote alikuwa ameiweka katika mfuko wa shati
alilokuwa amevaa.
Dawa alizokamatwa nazo zilikuwa kwa ajili ya matumizi yake, jeshi limeendelea kumshikiria mpaka Jumatatu kwa sababu leo (jana) na kesho (leo) sio siku za kazi
alisema.
Mbali ya dawa, msanii huyo alikutwa katika begi yake na kigae kidogo
cha chungu na kijiko, ikiwa ni maandalizi ya kutumia dawa hizo.
Msanii huyo alikuwa anakuja jijini Mbeya kwa shoo ya ‘Instagram
Party’ iliyofanyika jana katika ukumbi wa City Pub, jijini humo.
Chidi Benzi alikuwa ameongozana na msanii mwenzake Nurdin Bilal
‘Shetta’ ambaye naye alishikiliwa kwa muda kabla ya kuachiliwa kuendelea
na safari yake.
0 comments:
Chapisha Maoni