MKAZI wa kijiji cha Luteba, wilayani Rungwe mkoani Mbeya, jina linahifadhiwa (81)
amedaiwa kubakwa na watu wasiojulikana na kumsababishia maumivu makali.
Akisimulia mkasa huo Bibi huyo, alisema kuwa tukio hilo lilitokea
juzi usiku majira ya saa 8:00 wakati bibi huyo akiwa amelala nyumbani
kwake, ambapo alisikia kishindo cha watu ambao walimvamia na kumfunga
kitambaa usoni na kuanza kumuingilia kimwili.
Niliwaambia niwape hela wakasema hawana shida na kuniambia nikipiga kelele wataniua na ndipo walipoanza kunivua nguo kinguvu na kufanikiwa kunitendea unyama huo na na kuondoka na damu iliyokuwa ikinitoka
alisema
Alisema walipoondoka aliamua kupiga kelele za kuomba msaada kwa majirani waliompeleka katika kituo cha afya.
Mganga Mkuu wa kituo hicho Dk. Edwin Mwakisisya, alikiri kumpokea
Bibi huyo na kudai kuwa wanaendelea kumfanyia matibabu kwa lengo la
kumrudisha katika hali yake ya kawaida.
Akizungumza kwa niaba ya wazee wa makanisa wilayani humo mzee wa
kanisa la Baptist, Syemi Melele, alisema vitendo hivyo vimekuwa
vikijitokeza mara kadhaa na kwamba wanajipanga kuitisha makongamano
yatakayoendana na maombi kwa jamii hiyo ili iache vitendo hivyo.
Jeshi la polisi wilayani humo linaendele na uchunguzi wa kuwabaini wahusika wa tukio hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni