Ijumaa, Oktoba 17, 2014

CHANJO YA SURUA IRINGA

Wauguzi wa afya,‭ ‬viongozi wa dini na serikali zaidi ya‭ ‬30‭ ‬wa Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa wamepata mafunzo ya siku moja kuhusu chanjo ya ugonjwa wa surua ambayo inatarajia kutolewa kwa watoto mwezi huu.‭
Mkuu wa wilaya ya Iringa Dkt.‭ ‬Leticia Warioba amesema‭ ‬Mhe.‭Rais Jakaya Kikwete atazindua kampeni‭ ‬ya chanjo ya surua kwa‭ ‬watoto wa‭ ‬miezi‭ ‬9‭ ‬hadi miaka‭ ‬5‭ ‬mjini Dodoma Oktoba‭ ‬18‭ ‬mwaka huu ambapo kwa Mkoa wa Iringa itafanyika kwenye hospitari ya wilaya ya Frelimo Manispaa ya Iringa.‭ ‬
Dkt.‭ ‬Warioba amewashauri wananchi wa Manispaa na Mkoa wa Iringa kwa ujumla kuepukana na dhana ya kuwa chanjo mbalimbali ambazo hutolewa na serikali hupelekea kuzuia uzazi.
Kwa upande wa Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa Dkt.‭ ‬May Alexander amesema zaidi ya asilimia‭ ‬85‭ ‬ya watoto wameendelea kupata chanjo ya surua ambapo lengo la Manispaa likiwa ni kufikia asilimia‭ ‬100 ya watoto wote.
Dkt.‭ ‬Alexander ameongeza kuwa serikali imeongeza kasi ya kupambana na magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa ukoma,‭ ‬tauni,‭ ‬mabusha,‭ ‬matende,‭ ‬kichocho na minyoo ya tumbo ambayo awali yalikuwa hayapewi kipaumbele na yalikuwa yakiwaathiri watoto kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo,‭ ‬nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Mchg.‭ ‬Emso Sandagila wa kanisa la KKKT na Padre Anjero Pizzaia wa Parokia ya Mshindo Manispaa ya Iringa wameahidi kuhamasisha waumini wao juu ya umuhimu wa chanzo hiyo.‭

0 comments:

Chapisha Maoni