Polisi nchini Austria wanawahoji
wanawake ambao wamehadaiwa na mwanamume mwenye mazoea ya kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengi tu.
Mwanamume huyo raia
wa Gambia mwenye umri wa miaka 28 ameoa wanawake watatu huku akiwa
katika uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine 15
Kwa mujibu wa
mtandao wa 'ASN American street news', Tijan Sonko, alikamatwa tarehe
mbili mwezi Oktoba katika uwanja wa ndege mjini Vienna akiwa anarejea
kutoka nchini Gambia.
Pia anatuhumiwa kwa udanganyifu baada ya kuwapora wapenzi wake yuro 38,000.
Kadhalika ameshtakiwa na kosa la wizi na kutumia vitambulisho bandia.
Kulingana
na shirika la habari la Austria alitumia bima ya afya ya rafiki yake
kudai faida anazopata mtu ambaye hana ajira kutoka kwa serikali.
Mwanamke
mwenye umri mdogo sana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Sonko ana umri
wa miaka 22 huku mzee zaidi akiwa na umri wa miaka 44.
Msemaji wa
polisi mjini Vienna alisema kuwa wanawake wote waliohusika na Sonko
wanahojiwa kubaini ikiwa walidanganywa na kuibiwa.
Sonko alidai
kuwa alihitaji pesa ili kuwatumia jamaa wake nchini Gambia na wapenzi
wake kadhaa walimpa pesa na vifaa vingine vya thamani.
Ameishi mjini Vienna tangu Septemba mwaka 2010.
Udanganyifu
wake ulijulikana wakati wanawake wawili walijuana kupitia Facebook, na
kugundua kuwa walikuwa wanatoka na mwanamume mmoja.
Sonko ana watoto wanne mjini Vienna, na wapenzi wake wawili wanaaminika kuwa na mimba .
Ana mke nchini Gambia, na anaaminika kumpa zawadi na mapambo mengine aliyopewa na wapenzi wake wa Austria.
Tangu picha yake kuchapishwa na polisi, wanawake wengine wawili wamejitokeza wakisema na wao wamehadaiwa.
0 comments:
Chapisha Maoni