Ijumaa, Septemba 05, 2014

ZAIDI YA 30 WAFA KATIKA AJALI MARA

Inaelezwa kuwa ajali hiyo imehusisha magari matatu na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 30 na majeruhi wengi na imetokea
katika eneo la sabasaba maarufu kama kwa wachina takribani kilomita 25 kutoka Musoma mjini mkoani Mara.
Chanzo kimeeleza kuwa ajali hiyo imetokea wakati gari aina ya landcruiser kuingia barabarani ghafla, ndipo Basi la Mwanza Coach likitoka Musoma kwenda Mwanza likaivaa gari hiyo na wakati huo huo basi la AM Coach likitoka Mwanza kwenda Tarime nalo likagonga magari hayo.
Ajali hii imetokea majira ya saa 5 na nusu ,Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara,hospitali ya DDH Bunda na hospitali ya wilaya ya Butiama

0 comments:

Chapisha Maoni