Timu ya Young Africans itashuka dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam siku ya jumapili kucheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki wa
kimataifa dhidi ya timu ya Big Bullets FC (zamani Bata Bullets)
inayoshiriki Ligi Kuu ya TNM nchini Malawi.
Young Africans ambayo imeshacheza michezo minne mpaka sasa ya
kirafiki ukiwemo mmoja wa kimataifa katikati ya wiki hii dhidi ya timu
ya Thika United kutoka nchini Kenya imeshinda michezo yote.
Akiongea
na waandishi wa habari leo katika mkutano na waandishi wa habari, kocha
mkuu wa Young Africans mbrazil Marcio Maximo amesema mchezo huo wa siku
ya jumapili utakua ni kipimo kizuri kwa vijana wake kabla ya kuanza kwa
Ligi Kuu ya Vodacom wiki mbili zijazo.
Mchezo uliopita tuliocheza dhidi ya Thika United ulikua ni mchezo mzuri, tumepata nafasi ya kuyaona mapungufu yetu na kama mnavyofaham wenzetu wako katika Ligi inayondelea hivyo walicheza kitimu zaidi kuliko sisi na hata Big Bullets FC pia namini kitakua ni kipimo kizuri kwetu
alisema Maximo.
Kuhusu
timu ilivyocheza Maximo amesema hapendi kumzungumzia mchezaji mmoja
mmoja, na masula ya uchezaji hapendi kuyaongea kwa jamii, hiyvo yeye
kama kocha alishaongea na wachezaji na kuwaelezea mapungufu
yaliyojitokea na kipi wanapaswa kukifanya katika michezo inayofuata.
Aidha
Maximo aliongeza kuwa yeye kwa sasa hana kikosi cha kwanza, hana
mchezaji mwenye uhakika wa namba, kilichopo kwake ni kundi la wachezaji
ambao wote wana nafasi ya kucheza kulingana na mahitaji ya mchezo
wenyewe.
Afisa Habari wa Young Africans Bw Baraka Kizuguto amesema
taratibu zote za mchezo zimekamilika na timu ya Big Bullets FC kutoka
nchini Malawi inatarajiwa kuwasili kesho jijini Dar es salaam na kufanya
mazoezi jioni katika Uwanja wa Karume eneo la Ilala.
Mchezo wa jumapili tunatarajia utakua ni mchezo mzuri, ukizingatia timu ya Big Bullets FC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Malawi iiliyofikia mzunguko wa 17 kwa tofauti ya pointi moja na vinara, na kocha Maximo alipendekeza tupate timu tofauti kutoka ukanda wa Kusini mwa Afrika baada ya kuwa tayari tumeshacheza na timu ya Ukanda wa Afrika Mashariki
alisema Kizuguto.
Siku ya jumapili mechi
inatarijiwa kuanza majira ya saa 10 kwa saa za Afrika Mashariki na
viingilio vya mchezo ni kama ifuatavyo:
VIP A Tshs 30,000/=
VIP B & C Tshs 20,000/=
Orange Tshs 10,000/=
Blue & Green Tshs 5,000/=




0 comments:
Chapisha Maoni