Mkutano mkuu wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, umeadhimia
kuitisha na kuratibu,maandamano pamoja na migomo nchi nzima yasiyo kuwa
na ukomo, ili kushinikiza kusitishwa mara moja kwa shughuli za bunge
maalumu la katiba, linaloendela na vikao vyake mjini dodoma,na kuwagiza
wanasheria wake wote, kuandaa mashtaka,kwa wabunge wote wanaoendelea na
vikao vyao ndani ya bunge,kwa kufisadi fedha za walipa kodi watanzania.
Akitangaza maamuzi hayo jijini Dar-es-salaam,kwenye
mkutano mkuu wa tano wa Chadema,mwenyekiti wake Mh
Freeman Aikaeli Mbowe,amesema jitihada za mazungumzo baina ya wao ukawa
na viongozi wa juu wa serikali na chama tawala zimeonyesha kugongwa
mwamba kwa shughuli za bunge kuendela na vikao vyake mjini Dodoma.
Aidha Mh Mbowe amesema kuwa ,chama cha demokrasi na
maendelo Chadema, hakitamuonea haya kiongozi yeyote yule
atakayejihusiha na vitendo vya rushwa au kutowajibika kwa wananchi na
kuwa uongozi ni dhamana na hivyo kiongozi asiyewajibika kwa mujibu wa
katiba atang’olewa hata kama muda wake wa uongozi haujakamilika kwa
mujibu wa katiba.
Wakiongea kwenye mkutano huo viongozi wanaounda
umoja wa katiba ya wanachi Ukawa,kutoka vyama vikuu vya upinzani
nchini,CUF,NCCR-mageuzi pamoja na nld,ambapo kila mmoja kwa wakati wake
wamesema kuwa ili kung'oa ccm madarakani ni kuunganisha nguvu ya pamoja
kwa kumsimamisha mgombea moja ngazi ya urasi,na kuwa awali uoga na
kutokuaminiana ndivyo vilikuwa vinawasumbua,ambavyo sasa havipo.
Msajuli wa vyama vya siasa nchini,Profesa Fransice
Nutungi amewataka wanachadema kudumisha demokrasia waliyoinyesha wakati
wa mchakato mzima wa uchaguzi ndani ya chama hicho,kuanzia ngazi ya
chini hadi ngazi ya kitaifa na ndicho ambacho vyama vya siasa nchini
vinatakiwa kutekeleza jukumu hilo la kikatiba ndani ya vyama vya siasa.
Mkutano huo uliohudhuriwa na wageni mbalimbali
kutoka ndani na nje ya nchi,ambapo mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi ccm
Dkt Jakaya Kikwete pamoja na uongozi wa juu wa chama tawala
uliwakilishwa na makamu mwenyeikiti wa chama hicho tanzania bara bwana
philip mangula,ambapo amesema kwenye siasa ni kushindana kwa hoja bila
magonvi,yatakayopelekea uvunjifu wa amani iliyopo nchini.
0 comments:
Chapisha Maoni