Wakulima Mkoani Iringa wamekumbushwa kuandaa pembejeo za kilimo kwa wakati ili kuongeza uzalishaji kutokana kuwahi kwa msimu wa mvua zinazotaraji kuanza mapema mwezi novemba mwaka huu.
Mtaalamu wa Mamlaka ya hali ya Hewa kitengo cha kilimo toka mamlaka ya hali ya hewa {TMA} tawi la Iringa Bw. Edwin Kigenge amesema wakulima wanapaswa kuandaa mashamba yao mapema ili kupata mazao kwa wingi pindi mvua zitakapo anza.

Bw. Kigenge ameongeza kuwa, wananchi hususani wafugaji wanaokaa maeneo ya uoto wa asili wanatakiwa kutunza mazingira pamoja na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya malisho ya mifugo wao.
Naye Meneja wa kituo cha TMA tawi la Iringa Bw. Haji Usantu amesema wakulima na wafugaji kwa ujumla wanatakiwa kupandaji miti ya asili ambayo ni rafiki kwa mazingira ambayo itavumila hali ya kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande wa Mtafiti wa Mamlaka ya Hali ya Hewa kutoka Makao Makuu{TMA} Jijini Dar es Salaam Dkt. Ladislaus Chang'a amesema, wakulima wakijishughulisha na kilimo chenye tija pamoja na utunzaji wa mazingira itapelekea kupunguza athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Aidha amesema elimu ya utunzaji wa mazingira ikitolewa na kuwa endelevu kwa wananchi itasaidia uelewa kwa jamii na kupunguza changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Hata hivyo, Dkt Chang'a amesema mabadiliko ya hali ya hewa inatokana na ongezeko la gesi joto katika anga linalosababishwa na na shughuli za viwanda hasa kutoka nchi za zilizoendelea kiuchumi ikiwa ni pamoja na nchi za ulaya.1

0 comments:
Chapisha Maoni